Droo ya michuano ya African Football League (AFL) imekamilika na tumepangwa na miamba ya Afrika Al Ahly kutoka Misri.
Mchezo wa kwanza utapigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 20 ambao utatumika kama ufunguzi rasmi ya michuano hiyo.
Mechi ya marudiano itapigwa jijini Cairo, Misri Oktoba 24 ambapo mshindi wa jumla atatinga nusu fainali.
Mshindi wa baina yetu na Al Ahly atakutana na mshindi kati ya Petro Atletico ya Angola na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Droo kamili ilivyopangwa….
Simba vs Al Ahly
Mazembe vs Esperance
Enyimba vs Wydad
Petro De Luanda vs Mamelodi
Michuano hii itachezwa kwa muda wa wiki nne ambapo fainali ya kwanza itapigwa Novemba 5 na ile ya pili itapigwa Novemba 11.