Droo ya upangaji makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika imekamilika jijini Cairo, Misri ambapo timu yetu tumepangwa Kundi C.
Katika kundi letu tumepangwa pamoja na miamba ya Soka barani Afrika Raja Casablanca ya Morocco, Horoya ya Guinea pamoja na Vipers kutoka Uganda.
Mechi za hatua ya makundi zitaanza kupigwa kati ya Februari 10 hadi Aprili Mosi mwakani.
Kundi C
Raja Casablanca (Morocco)
Horoya AC (Guinea)
Simba SC (Tanzania)
Vipers SC (Uganda)