Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mashujaa FC uliopigwa katika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma umemalizika kwa kufanikiwa kupata ushindi wa bao moja.
Mchezo huo ulianza kwa kasi huku tukifika zaidi katika lango la Mashujaa lakini tulipoteza umakini wa kutumia nafasi tulizotengeneza.
Saido Ntibazonkiza alitupatia bao la kwanza dakika ya 14 kwa mkwaju wa penati baada ya Kibu Denis kufanyiwa madhambi ndani ya 18.
Kipindi cha pili tuliongeza kasi ya kuliandama lango la Mashujaa lakini changamoto ikawa ile ile kutumia nafasi tulizopata.
X1: Johora, Abrahaman, Mwakinyuke, Ame, Madereke, Mtuwi, Omary, Dabi, Lusajo, Adam, Balama.
X1. Manula, Israel, Zimbwe Jr, Kazi, Che Malone, Sarr, Kibu (Miqussone 81′), Mzamiru (Chama 74′), Fred (Pa Jobe 81′), Kanoute (Kapombe 90+2), Ntibazonkiza (Hamis 92+2)
Walioonyeshwa kadi: Kanoute 70′