Mchezo wetu wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Black Stars uliopigwa Uwanja wa Liti umemalizika kwa ushindi wa bao moja.
Tulianza mchezo kwa kasi huku tukifika zaidi langoni mwa Singida lakini mashambulizi yetu yaliishia kwa walinzi pamoja na mlinda mlango, Metacha Mnata.
Fabrice Ngoma alitupatia bao hilo pekee dakika ya 41 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Jean Charles Ahoua.
Kipindi cha pili kasi ya mchezo iliongezeka huku Singida nao wakifika langoni kwetu mara kadhaa lakini mlinda mlango Moussa Camara alikuwa imara.
Ushindi huo umetufanya kufikisha pointi 40 tukiwa kileleni mwa msimamo baada ya kucheza mechi 15.
X1: Metacha, Ande, Imoro (Manyama 63′), Kennedy, Trabi, Damaro, Khalid (Adebayor 75′), Keyekeh, Arthur, Tchakei (Lyanga 63′), Rupia
Walioonyeshwa kadi: Tchakei 18′ Imoro 21′ Kennedy 58′
X1: Camara, Kapombe, Zimbwe Jr (Chamou 70′), Hamza, Che Malone, Kagoma, Kibu, Ngoma, Mukwala (Ateba 90′) Mpanzu (Awesu 70′), Ahoua (Fernandez 80′)
Walioonyeshwa kadi: Kagoma 65′