Tumejipanga kuanza vizuri Kombe la Shirikisho

Kocha Mkuu, Fadlu Davids amesema licha ya ubora na ugumu wa wapinzani wetu Bravo Do Marquis kutoka Angola lakini tumejipanga kuhakikisha tunaanza vizuri michuano ya Kombe la Shirikisho kwa ushindi kesho.

Kocha Fadlu amesema tumepata siku nne za kufanya mazoezi tangu tulivyocheza mechi ya ligi ya mwisho dhidi ya Pamba Jiji na wachezaji wapo kwenye hali nzuri.

Kocha Fadlu ameongeza kuwa itakuwa ni jambo jema kwetu kuanza kwa ushindi hasa tukiwa nyumbani ingawa haitakuwa kazi kubwa lakini tumejipanga na tupo tayari.

“Ni mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho ambao tunacheza katika Uwanja wa nyumbani ni muhimu kwetu kupata ushindi na kuwafurahisha mashabiki.

“Tunatarajia mashabiki wetu watajitojeza kwa wingi kutushangalia. Tumepangwa kundi gumu lakini ndio muda wa kuonyesha ukubwa wetu,” amesema Kocha Fadlu.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa kati, Che Fondoh Malone amesema kwa upande wao wapo tayari na kila atayepata nafasi amejipanga kufanya vizuri.

“Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu lakini tupo nyumbani na tuna faida yakucheza mbele ya mashabiki wetu na tumejiandaa kuwapa furaha,” amesema Che Malone.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER