Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kengold uliopigwa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora umemalizika kwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0.
Kibu Denis alitupatia bao la kwanza dakika ya 20 kwa shuti kali nje ya 18 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Kengold.
Elie Mpanzu alitupatia bao la pili dakika ya 22 kwa shuti kali nje ya 18 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Kibu.
Dakika ya 25 Kibu alitupatia bao la tatu kwa shuti kali akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Jean Charles Ahoua.
Leonel Ateba alitupatia bao la nne dakika ya 36 baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Mpanzu.
Ahoua bao la tano dakika 75 baada ya kumalizia pasi safi iliyopigwa na Ateba akiwa nje kidogo ya 18.
Matokeo haya yanatufanya kufikisha alama 75 baada ya kucheza mechi 28 tukiendelea kusalia nafasi ya pili.
X1: Lonje, Gabriel, Makhenzi, Kazila, Yondani (Robert 82′), Lipangile, Lukindo (Kayanda 65′), Chirwa (Mpuka 54′) Manyinyi, Morrison Ambukege
Waliionyeshwa kadi:
X1: Camara, Kapombe (Duchu 61′), Zimbwe Jr, Chamou (Nouma 61′), Che Malone, Kagoma (Okajepha 45′), Kibu (Mukwala 78′) Deborah, Ateba, Ahoua, Mpanzu (Mutale 61′)
Waliionyeshwa kadi: