Tumeibuka na ushindi dhidi ya Coastal

Mchezo wetu wa kutafuta mshindi wa tatu wa Ngao ya Jamii dhidi ya Coastal Union uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa umemalizika kwa kupata ushindi wa bao moja.

Saleh Karabaka alitupatia bao hilo pekee dakika ya 11 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Joshua Mutale.

Baada ya bao hilo tuliendelea kuliandama lango la Coastal huku tukimiliki sehemu kubwa ya mchezo ingawa hatukuweza kutumia nafasi tulizopata.

Kipindi cha pili Coastal walirudi kwa kasi na kufanya mashambulizi mengi langoni kwetu lakini idara yetu ya ulinzi ilikuwa imara.

Kiungo mkabaji Fabrice Ngoma alitolewa dakika ya 84 baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kufuatia kumchezea madhambi Mbaraka Yusuph.

X1: Camara, Kijili, Zimbwe Jr (Nouma 66′), Che Malone, Hamza, Okajepha, Karabaka, Fernandes (Balua 56′), Mukwala (Mashaka 56′), Ahoua (Ngoma 56′), Mutale (Kibu 80′)

Walioonyeshwa kadi: Ngoma 79′ 84′ Valentino 87′

X1: Chuma, Jackson, Miraji, Issa, Abdallah, Semfuko, Denis (Gwalala 45′), Ranadhani, John (Mbaraka 80′), Lucas (Cosmas 64′), Hernest (Banza 80′) (Hassan 45′)

Walioonyeshwa kadi: Gwalala 89′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER