Tumechukua Pointi zote za KMC

Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC uliopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha umemalizika kwa kuibuka na ushindi wa bao moja.

Mchezo huo uliokuwa mkali na kuvutia muda wote bao letu pekee limefungwa na Saido Ntibazonkiza dakika ya tatu baada ya kumzidi ujanja mlinda mlango wa KMC, Denis Richard.

Baada ya bao hilo mchezo uliendelea kuwa wa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini hakukuwa na ufanisi katika eneo la mwisho.

Kipindi cha pili timu zote zilirudi kwa kasi huku mpira ukichezwa zaidi eneo la katikati ya uwanja.

Kocha Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwatoa Willy Onana, Ladaki Chasambi na Ntibazonkiza na kuwaingiza Edwin Balua, Luis Miqussone na Saleh Karabaka.

Ushindi huu unatufanya kufikisha pointi 66 tukiendelea kusalia nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER