Bao la dakika ya mwisho lililofungwa kwa mkwaju wa penati na kiungo mshambuliaji Jean Charles Ahoua limetuwezesha kutupa ushindi dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa KMC Complex.
Ahoua alifunga bao hilo dakika ya tano ya nyongeza kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi David Bryson kuunawa mpira ndani ya 18 akiwa katika harakati za kuokoa.
Tulianza mchezo kwa kasi huku tukishambulia lazidi lango la JKT lakini kikwazo kikubwa kilikuwa mlinda mlango, Yakubu Mohamed.
Kiungo mshambuliaji, Elie Mpanzu alifanya jitihada za kuipambania timu kupata bao la uongozi lakini hata hivyo mashuti yake matatu yaliishia mikononi mwa Yakubu.
Kiungo mshambuliaji Mohamed Bakari alitolewa baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya tano ya nyongeza baada ya kumchezea madhambi Shomari Kapombe ndani ya 18.
Ushindi huu umetufanya kufikisha pointi 37 baada ya kucheza mechi 14 tukiendelea kuwa kileleni mwa msimamo.
X1: Camara, Kapombe, Nouma (Zimbwe Jr 70′), Che Malone, Hamza, Ngoma, Awesu (Ahoua 45′) Fernandez (Mashaka 77′) Ateba (Mukwala 59′), Mpanzu (Mutale 59′), Chasambi
Walioonyeshwa kadi:
X1: Yakubu, Salim, Wilson, Nagu, Bryson, Kapalata, Ndemla (Dilunga 65′), Maguru (Matheo 65′), Kataga, Matiko (Bocco 77′), Shiza (Mohamed 65′), Machezo (Bausi 89′)
Walioonyeshwa kadi: Machezo 34′ Nangu 43′ Yakubu 71′ Mohamed Bakari 76′ 90+2 Dilunga 90+3