Tumechukua alama tatu za Dodoma kibabe

Tumefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa katika Uwanja wa KMC Complex.

Elie Mpanzu alitupatia bao la kwanza dakika ya 15 kwa shuti kali nje ya 18 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Kibu Denis.

Jean Charles Ahoua alitupatia bao la pili dakika ya 21 kwa shuti la chini chini akiwa ndani ya 18 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’.

Ahoua alitupatia bao la tatu dakika ya 45 kwa shuti kali akiwa ndani ya 18 baada ya kumalizia pasi safi iliyopigwa na Kibu.

Steven Mukwala alitupatia bao la nne kwa kisigino dakika ya 46 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Mpanzu.

Kibu alitupatia bao la tano dakika ya 54 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Mpanzu.

Kibu alitupatia bao la sita dakika ya 69 akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Ahoua.

Ushindi huu unatufanya kufikisha pointi 57 tukiwa nafasi ya pili kwenye msimamo tukizidiwa alama moja na vinara.

X1: Ally (Abel 61′), Duchu (Kijili 82′) Zimbwe Jr (Nouma 82′) Chamou, Hamza, Kagoma, Kibu, Ngoma (Mavambo 61′) Mukwala (Ateba 77′) Ahoua, Mpanzu

Waliionyeshwa kadi: Hamza 86′

X1: Ngeleka, Augustino, Apollo, Hoza (Banda 49′) Milandu (Mwaterema 49′), Mwana, Mhilu, Mukrimu, Lusajo, Obata (Ajibu 49′) P. Peter

Waliionyeshwa kadi:

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER