Tumechukua alama tatu kutoka kwa Ken Gold

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ken Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa KMC Complex.

Tulianza mchezo kwa kasi huku tukifanya mashambulizi mengi langoni mwa Ken Gold katika dakika 20 za mwanzo lakini tulikosa ufanisi wa kutumia nafasi tulizopata.

Leonel Ateba alitupatia bao la kwanza dakika ya 34 kwa mkwaju wa penati baada ya kiungo mshambuliaji Awesu Awesu kufanyiwa madhambi ndani ya 18 na kiungo mkabaji George Sangija.

Ateba alitupatia bao la pili kwa kichwa dakika ya 44 baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na mlinzi wa kushoto, Valentine Nouma.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini lakini tulikosa ufanisi wa kuzitumia.

Ushindi huu unatufanya kurejea kwenye kilele cha msimamo wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kufikisha alama 31 baada ya kucheza mechi 12.

X1: Camara, Kijili (Zimbwe Jr 72′), Nouma, Chamou, Che Malone, Mzamiru (Okajepha 55′), Chasambi(Mutale 72′), Ngoma (Kagoma 45′), Ateba, Awesu (Ahoua 55′) Kibu

Walioonyeshwa kadi:

X1: Castro, Mwaipopo, Bilal, Kazila, Lubinda, Sangija, Daud, Cabaye, Joshua (Abdallah 74′), Hamad (Faraji 58′), Lukindo (Ugando 74′)

Walioonyeshwa kadi: Kazila 23′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER