Kikosi chetu cha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kimeanza kwa sare ya bila kufungana na Kagera Sugar katika michuano ya vijana ambayo imeanza jana mtanange uliopigwa Uwanja wa Azam Complex.
Mchezo huo ulianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu huku mchezo ukichezwa zaidi katikati ya uwanja.
Mechi hiyo ambayo imehudhuriwa na mashabiki wengi ilitawaliwa na mbinu zaidi za makocha kitu kilichokuwa kinavutia.
Kipindi cha pili kila timu ilitengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini changamoto ikawa kwenye kuzitumia.
Baada ya mchezo wa leo kikosi chetu kitashuka tena dimbani Jumamosi kuikabili Ihefu FC.