Tuko tayari kuikabili Namungo Kesho

Kocha Msaidizi Seleman Matola amesema kikosi kiko tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu dhidi ya Namungo FC utakaopigwa katika Uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa mkoani Lindi saa 10 jioni.

Matola amesema wachezaji wote 20 waliosafiri wako vizuri kiafya na kila mmoja yupo kwenye nafasi nzuri ya kushuka dimbani kuikabili Namungo.

Kikosi kiliwasili Ruangwa leo Ijumaa Mei 28, saa tano asubuhi ambapo leo jioni kitafanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Majaliwa kabla ya kesho kushuka dimbani.

Matola ameongeza kuwa tunafahamu mchezo utakuwa mgumu, Namungo ni timu nzuri hasa inapokuwa nyumbani lakini lengo letu ni kuhakikisha tunashinda kwenye kila mchezo.

“Tunamshukuru Mungu tumefika salama hapa Lindi, wachezaji wote wako vizuri. Tunajua haitakuwa mechi rahisi Namungo ni timu nzuri hasa inapocheza nyumbani lakini sisi  tumejipanga kuondoka na alama zote,” amesema Matola.

Matola amesema katika mchezo wa kesho tutakosa huduma ya wachezaji Joash Onyango, Clatous Chama na Ibrahim Ame kutokana na sababu tofauti.

“Tutakosa huduma ya Onyango ambaye bado afya yake haijaimarika vizuri, Chama ameaga ana matatizo ya kifamilia na Ame anayetumikia adhabu ya kufungiwa,” amesema Matola.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER