Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu, Salim Abdallah ‘Try Again’ leo ameongoza kikao cha Bodi kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya klabu.
Kikao cha leo ni cha kwanza cha Bodi ya Wakurugenzi kwa Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo miezi mitatu iliyopita.
Pia kikao hicho ni cha kwanza kwa Wajumbe wapya wa Bodi waliochaguliwa na wanachama pamoja na wale walioteuliwa na muwekazaji Mohamed Dewji ‘Mo’.