Kikosi cha timu yetu ya vijana kitashiriki michuano ya Ligi Kuu chini ya umri wa miaka 20 ambayo itaanza kutimua vumbi Julai mwaka huu.
Michuano hiyo itahusisha timu zote 16 za vijana ambazo timu zake kubwa zinashiriki Ligi Kuu ya NBC.
Timu hizo zimegawanywa kwenye makundi manne yenye timu nne kila moja ambapo sisi tumepangwa kundi A.
Kundi letu lipo kama ifuatavyo
Simba
Polisi Tanzania
Biashara United
Namungo FC
Katika michuano hiyo mwaka jana tulimaliza nafasi ya tatu baada ya kuifunga Azam FC kwa mikwaju ya penati 4-1 baada ya sare ya bao moja katika muda wa kawaida wa dakika 90.