Kikosi chetu kimewasili salama katika mji wa Tunis nchini Tunisia kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya CS Sfaxien utakaopigwa Januari 5.
Kikosi kimeondoka jijini Dar es Salaam alfajiri ya leo kikipitia Instanbul, Uturuki kabla ya kuunganisha Ndege kuelekea Tunisia.
Timu imeondoka na msafara wa watu 50 huku wachezaji wakiwa 22 ambao tunaamini wapo tayari kuipambania timu kupata matokeo chanya.
Kikiwa hapa Tunisia kikosi chetu kitapata nafasi ya kufanya mazoezi kwa siku tatu huku kikizoea hali ya hewa.
Mchezo huo ambao utapigwa Januari 5 saa moja usiku kwa saa za Tanzania hautakuwa na mashabiki kutokana na CS Sfaxien kufungiwa baada ya kufanya vurugu viwanjani.