Kikosi chetu kimewasili salama mkoani Tabora tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kengold utakaopigwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi saa 10 jioni.
Kikosi kimeondoka jijini Dar es Salaam asubuhi kwa usafiri wa treni ya Mwendokasi SGR na kupitia Dodoma kabla ya kuchukua basi mpaka Tabora.
Baada ya kuwasili Tabora saa 11 kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kujiweka sawa kabla ya kushuka dimbani kesho.