Kikosi chetu kimewasili salama mkoani Kagera tayari kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi wa Ligi kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa katika Uwanja wa Kaitaba saa 10 jioni.
Tumesafiri na wachezaji 24 ambao tunaamini wapo tayari kupambana kwa ajili ya kutupatia alama tatu muhimu ugenini.
Baada ya kufika kikosi kitafanya mazoezi ya utimamu wa mwili kutokana na uchovu wa safari na baadae kuendelea na programu Kamili.