Kikosi chetu kimewasili salama katika mji wa Francis Town ambapo ndio mchezo wetu wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United utakaopigwa Jumamosi saa mbili usiku.
Kikosi kimefika jana nchini Botswana lakini leo kimewasili katika mji wa FrancisTown kutakapochezwa mchezo wetu.
Baada ya kufika FrancisTown Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya utimamu wa mwili kutokana na uchovu wa safari.
Kesho jioni Kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho katika uwanja Obedi Itani Chilume ambao ndio tutautumia katika mchezo wetu wa Jumamosi.