Timu yawasili salama Casablanca

Kikosi chetu kimewasili salama jijini Casablanca nchini Morocco kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane utakaopigwa Jumamosi, Mei 17.

Msafara huo umejumuisha viongozi kutoka Serikalini, Viongozi kutoka Menejimeti, Benchi la Ufundi, wachezaji na mashabiki.

Kikosi kitaweka kambi ya siku mbili hapa Casablanca kabla ya kuelekea katika mji wa Oujda ambapo kutapigwa mchezo huo wa mkondo wa kwanza.

Pamoja na kuwaheshimu Berkane kwa ubora na uzoefu wao kwenye michuano hii Jumamosi tutaingia uwanjani kwa malengo ya kuhakikisha tunapata matokeo chanya.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER