Timu yawasili salama Arusha

Kikosi chetu kimewasili salama jijini Arusha tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC utakaopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid saa 10 jioni.

Kikosi kimeondoka na jumla ya wachezaji 22 tayari kwa mchezo huo ambao tunategemea kuwa mgumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

Uongozi wa klabu unaendelea kuwaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi uwanjani ili kuipa sapoti timu ili kupata matokeo chanya.

Tayari viingilio vya mchezo vimetangazwa na vipo kama ifuatavyo:

VIP A Sh. 30,000
VIP B Sh. 15,000
Mzunguko Sh. 10,000

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER