Kikosi chetu kimefika salama nchini Angola kwa ajili ya mchezo wa tano wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bravos Do Marquis utakaopigwa Jumapili katika Uwanja wa Novemba 11.
Kikosi kiliondoka jijini Dar es Salaam alfajiri kikipitia Ethiopia kabla ya kuunganisha hadi hapa Angola.
Baada ya kikosi kufika kimeelekea hotelini ili wachezaji waweze kupumzika kwa saa chache kabla ya kufanya mazoezi ya utimamu baada ya safari ndefu.
Kocha Mkuu Fadlu Davids ataendelea na programu ya mazoezi kesho pamoja na keshokutwa kabla ya Jumapili kushuka dimbani.