Timu yarejea salama Dar

Kikosi chetu kimewasili salama jijini Dar es Salaam kutoka Tunisia baada ya mchezo wa nne wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi dhidi ya CS Sfaxien ambao tumeibuka na ushindi wa bao moja siku ya Jumapili.

Kikosi kiliondoka nchini Tunisia jana asubuhi  kupitia Uturuki kilipounganisha ndege hadi jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuwasili timu itaanza mara moja maandalizi ya mchezo unaofuata wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bravos Do Marquis ya Angola utakaopigwa Januari 12.

Mchezo dhidi ya Bravos utapigwa katika Uwanja wa Novemba 11 nchini Angola saa moja usiku kwa saa za Tanzania.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER