Timu yarejea mazoezini kujiandaa na Bigman FC

Kikosi chetu leo kimerejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa hatua ya 16 bora ya CRDB Federation Cup utakaopigwa Machi, 27 katika Uwanja wa KMC Complex saa 10 jioni.

Baada ya ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Dodoma Jiji, Machi 14 wachezaji walipewa mapumziko ya siku chache.

Mara baada ya kumalizika mchezo dhidi ya Bigman kikosi kitaanza safari ya kuelekea Misri kwa ajili ya mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry utakaopigwa Aprili 2.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER