Timu yarejea kutoka Zanzibar, yaanza maandalizi

Kikosi chetu kimerejea jijini Dar es Salaam kutoka Zanzibar baada ya mchezo wa jana wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch tulioibuka na ushindi wa bao moja.

Baada ya kufika Dar es Salaam mchana wachezaji wamepewa mapumziko ya saa chache ambapo jioni watafanya mazoezi ya Gym kuweka miili sawa.

Kuanzia leo kikosi kitaendelea na maandalizi ya mchezo wetu wa marudiano wa nusu fainali ya dhidi ya Stellenbosch utakaopigwa Jumapili nchini Afrika Kusini.

Mchezo huo utapigwa saa 10 jioni katika Uwanja wa Moses Mabhida katika mji wa Durban.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER