Timu yarejea Dar Wachezaji wapewa mapumziko

Kikosi kimewasili salama asubuhi kutoka nchini Morocco baada ya mchezo wa tatu wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca tuliocheza Jumamosi usiku.

Baada ya kufika wachezaji wamepewa mapumziko na kesho wataanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Ijumaa, Disemba 15 jijini Dar es Salaam.

Pamoja na uchovu kutokana na umbali wa safari kutoka Morocco wachezaji hawajapewa muda mwingi wa kupumzika kwakuwa tuna ratiba ngumu iliyopo mbele yetu.

Baada ya mechi dhidi ya Kagera siku ya Ijumaa siku tatu baadae tutakuwa na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER