Timu yaingia kambini kujiwinda na Orlando

Kikosi chetu kimeingia kambini baada ya mazoezi ya asubuhi tayari kwa maandalizi ya mchezo wetu wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates utakaopigwa nchini Afrika Kusini wikiendi ijayo.

Baada ya ushindi wa bao moja tuliopata katika uwanja wa nyumbani Jumapili, jana wachezaji walipewa mapumziko na leo kikosi kimeanza mazoezi na kuingia kambini moja kwa moja.

Tumeanza mazoezi mapema kwa kuwa lengo letu ni kuhakikisha tunapata matokeo mazuri ugenini ili kufuzu hatua ya nusu fainali.

Morali ya wachezaji ipo juu na hakuna aliyepata majeraha makubwa katika mchezo wetu wa kwanza tunamuomba Mungu waendelee kuwa salama mpaka katika mechi yetu ya marudiano.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER