Kikosi chetu leo kimengia kambini rasmi kujiandaa na mchezo wa tatu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC utakaopigwa Jumatano Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.
Wachezaji 10 waliokuwa kwenye majukumu ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) nao wameungana na wenzao tayari kwa maandalizi ya mtanange huo.
Kikosi kitafanya mazoezi saa 10 jioni katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena kuendelea kujiandaa mtanange huo.
Dhamira yetu ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo hasa wa nyumbani ili kukusanya alama nyingi kwakuwa tunahitaji kurejesha mataji yetu.