Timu yahamishia kambi jijini Cairo

Baada ya kuweka kambi kwa siku 15 katika mji wa Ismailia kikosi chetu leo kimehamia jijini Cairo kuendelea na maandalizi ya msimu mpya wa mashindano 2025/2026.

Wakati kikiwa katika kambi ya Ismailia kikosi kimefanikiwa kucheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya Karhaba Ismailia SC na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Baada ya kufika Cairo kikosi kitaendelea na programu ya mazoezi kwa siku nyingine 15 kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam.

Kikiwa kambini jijini Cairo kikosi kinatarajia kucheza mechi kadhaa za kirafiki ili kuliwezesha benchi la ufundi kuona jinsi wachezaji walivyoshika mafunzo wanayopewa.

Kikosi kitarejea jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi huu tayari kuanza msimu mpya wa Ligi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER