Timu yafika salama Morocco

Kikosi chetu kimewasili salama nchini Morocco tayari kwa mchezo wa kesho wa marudiano wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca utakaopigwa saa 7 usiku kwa saa za Tanzania.

Kikosi kimewasili nchini Morocco saa tatu asubuhi ambapo huku kwetu ni saa sita mchana huku wachezaji wakiwa kwenye hali nzuri.

Wachezaji wanne waliokuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Aishi Manula, Beno Kakolanya, Mzamiru Yassin na Shomari Kapombe ambao waliondoka nchini jana mchana walikutana na kikosi Qatar na kuunganisha pamoja mpaka Morocco.

Wachezaji wakimataifa walifika Morocco toka jana usiku na kikosi tayari kiko kamili kwa ajili ya mchezo wa kesho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER