Kkosi chetu kimefanya mazoezi ya utimamu wa mwili asubuhi baada ya mchezo wa jana wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC.
Katika mchezo wa jana hatukupata majeruhi yoyote hivyo wachezaji na wote wameshiriki mazoezi hayo.
Baada ya Mazoezi kikosi kitarejea jijini Dar es Salaam mchana na moja kwa moja kitaingia kambini.
Kesho asubuhi kikosi kitaanza safari ya kuelekea jijini Dodoma kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa Jumapili katika Uwanja wa Jamhuri.