Timu yafanya mazoezi ya mwisho Uhuru

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho asubuhi katika Uwanja wa Uhuru ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi Azam FC utakaopigwa kesho saa moja usiku Uwanja wa Azam Complex.

Ni wachezaji wawili tu Clatous Chama na Jonas Mkude ambao hawajafanya mazoezi hayo kutokana na kuwa majeruhi lakini wengine wapo fiti.

Morali ya wachezaji ipo juu na kila mmoja amejitahidi kujituma mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi kesho.

Kwa sasa kila mchezo kwetu ni fainali tunahitaji alama tatu ili kuendelea kupunguza tofauti ya pointi iliyopo baina yetu na wanaoongoza.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER