Timu yafanya mazoezi ya mwisho Sokoine

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Sokoine tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa kesho saa 10 jioni.

Tumesafiri na wachezaji 22 na wote wameshiriki mazoezi kikamilifu na hakuna aliyepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo wa kesho.

Baada ya mazoezi kocha Mkuu Fadlu Davids amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo.

Kocha Fadlu amesema tunatarajia kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Prisons lakini tupo tayari kwa ajili ya kupigania pointi tatu.

“Tumefanya mazoezi ya mwisho jioni katika Uwanja wa Sokoine na tupo tayari kwa ajili ya mechi ya kesho,” amesema Kocha Fadlu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER