Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mazoezi hayo yameongozwa na kocha mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ pamoja na wasaidizi wake wa benchi la ufundi.
Wachezaji wamejitahidi kuonyesha jitihada na uwezo mkubwa mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kuwapa nafasi katika mchezo wa kesho.
Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu kutokana na ubora wa Coastal na tunawaheshimu lakini nasi tumejipanga kikamilifu kuhakikisha tunapata alama zote tatu nyumbani.