Timu yafanya mazoezi ya mwisho Mo Arena

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union utakaopigwa kesho.

Mchezo huo ambao utapigwa katika Uwanja wa Azam Complex saa 10 jioni tunatajia utakuwa mgumu lakini kwakuwa tupo nyumbani tunaamini tutapata ushindi.

Awali wakati akiongea na Waandishi wa Habari Kocha, Mkuu Fadlu Davids amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri huku akiweka wazi anatarajia kufanya mabadiliko kidogo ya kikosi kutokana na ratiba kuwa ngumu.

“Siwezi kusema nitampanga mchezaji gani au nani hatakuwepo kesho kwakuwa ratiba ni ngumu. Tunatengeneza uwiano wa wachezaji kwakuwa kuelekea Disemba ratiba itakuwa ngumu zaidi kwahiyo kila mmoja anatakiwa kupata muda wa kucheza,” amesema Kocha Fadlu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER