KIkosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena kabla ya kesho kuanza safari ya kuelekea Zanzibar kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Azam FC.
Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na hakuna yeyote ambaye amepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo huo.
Kikosi kitaondoka kesho kikiwa na wachezaji 22 tayari kwa mchezo huo ambao utapigwa katika Uwanja wa New Amaan Complex Alhamisi saa 2:30 usiku.
Mchezo huo utakuwa ni wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC kupigwa Zanzibar nasi tumejipanga kuhakikisha tunaanza kwa ushindi.
Tunaondoka tukiwa na kumbukumbu ya ushindi mnono wa mabao 3-1 tuliopata dhidi ya Al Ahli Tripoli ambao umetuwezesha kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.