Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena kabla ya kesho kuanza safari ya kuelekea Libya tayari kwa mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Ahly Tripoli.
Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri huku lengo likiwa ni kuisaidia timu kufika hatua ya makundi.
Morali za wachezaji zipo juu na kila mmoja amejitahidi kuonyesha uwezo wake mazoezini hali inayoonesha tupo tayari kwa mchezo huo.
Kikosi kitaondoka kesho Alfajiri kikipitia Uturuki ambapo kitapumzika kwa siku nzima kabla ya kuelekea Libya.