Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena asubuhi kujiandaa na mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi saa 10 jioni.
Katika mazoezi hayo ambayo yamesimamiwa na Kocha Juma Mgunda na wasaidizi wake wachezaji wameonyesha jitihada kubwa na wameonekana wapo tayari kwa mchezo wa kesho.
Mzamiru Yassin ambaye aliukosa mchezo uliopita dhidi ya Namungo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano nae ameshiriki mazoezi hayo na yupo tayari kwa mchezo wa kesho.