Timu yafanya mazoezi ya mwisho Mo Arena

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi KMC utakaopigwa Azam Complex saa 10 Jioni.

Wachezaji wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu chini ya Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha huku wakikosekana Clatous Chama na Nassor Kapama waliosimamishwa.

Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda ili kuendelea kukusanya pointi tatu.

Mara zote KMC wamekuwa wakitupa ushindani mkubwa kutokana na ubora walionao lakini hata hivyo tupo tayari kuwakabili.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER