Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Kimataifa wa Tripoli tayari kwa mchezo wa kesho wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya kwanza dhidi ya Al Ahli Tripoli.
Mazoezi hayo yamefanyika usiku muda ambao mchezo huo utapigwa ambapo kwa Libya itakuwa ni saa moja na nyumbani Tanzania itakuwa ni saa mbili usiku.
Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo huo ambao tunaamini utakuwa mgumu.
Morali za wachezaji zipo juu na kila mmoja amejitahidi kuonyesha uwezo kwa walimu ili kupata nafasi ya kuanza kwenye mchezo wa kesho.