Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho jioni katika Uwanja wa Orlando kujiandaa na mchezo wa robo fainali ya pili ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates utakaopigwa kesho saa moja usiku.
Tutaingia katika mchezo wa kesho tukiwa na faida ya bao moja tulilopata katika mchezo wa kwanza hivyo sare ya aina yoyote itatufanya kutinga nusu fainali.