Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa KMC kujiandaa na mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tabora United utakaopigwa kesho saa 10:15 jioni.
Wachezaji wote wameshiriki kikamilifu mazoezi hayo na wapo tayari kwa mchezo wa kesho ambao tunahitaji alama tatu muhimu.
Mapema mchana wa leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari Kocha Mkuu Fadlu Davids ameweka wazi kuwa malengo ya timu ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo.
Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu kutokana na ubora wa Tabora lakini tumejiandaa vizuri kuwakabili.