Timu yafanya mazoezi ya mwisho Kigoma

Nyota wote 26 tuliosafiri nao kuja Kigoma kwa ajili ya mchezo wa kesho wa hatua ya 16 bora ya CRDB Bank Federation Cup dhidi ya Mashujaa FC wameshiriki mazoezi ya mwisho jioni yaliyofanyika Uwanja wa Lake Tanganyika.

Kikosi kiliwasili Kigoma leo mchana na wachezaji walipata saa chache za kupumzika kabla ya jioni kufanya mazoezi ya hayo ya mwisho yaliyoongozwa na Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha.

Katika mazoezi hayo hakuna mchezaji aliyepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo wa kesho.

Morali za wachezaji zipo juu na kila mmoja amejitahidi kuonyesha uwezo wake mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi katika mchezo wa kesho.

Mchezo wa kesho tunaupa umuhimu mkubwa na tunahitaji kupata ushindi ili kufuzu robo fainali kwakuwa moja ya malengo yetu msimu huu ni kutwa taji la michuano hii.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER