Timu yafanya mazoezi ya kwanza nchini Misri

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya kwanza usiku huu nchini Misri ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa robo fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry utakaopigwa Jumatano Aprili 2.

Mazoezi hayo yamefanyika katika viwanja vya Hoteli tuliyofikia ya Tolip Hotel Resort ambapo wachezaji wote wameshiriki.

Nyota sita waliokuwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania waliocheza dhidi ya Morocco siku ya Jumatano walikuwa wakwanza kufika Misri na wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu.

Kwa mujibu wa ratiba kikosi kitaendelea kufanya mazoezi usiku ili kuendelea kuzoea mazingira ya hali ya hewa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER