Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho jioni katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa hatua ya 32 bora ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya TRA utakaopigwa kesho Uwanja wa Azam Complex saa moja usiku.
Tunauchukulia kwa umuhimu mkubwa mchezo wa kesho na tutaingia kwa tahadhari huku tukiwaheshimu TRA lengo likiwa kuhakikisha tunashinda na kutinga hatua ya 16 bora.
Tunawaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kesho katika mchezo huo kwa ajili ya kuipa sapoti timu ili tufanikishe malengo ya kutinga katika hatua hiyo.