Timu yaendelea na mazoezi Mo Arena

Kikosi chetu kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya watani wetu Yanga utakaopigwa dimba la Benjamin Mkapa Jumapili.

Timu iliingia rasmi kambini jana kujiandaa na mchezo huo ambao unavuta hisia za mashabiki wengi ndani na nje ya nchi.

Wachezaji wote walioshiriki mchezo wetu wa mwisho dhidi ya Premiero De Agosto mwishoni mwa juma lililopita wameingia kambini na wameshiriki mazoezi ya leo.

Morali ya wachezaji ipo juu na wanafanya kila linalowezekana kulishawishi benchi la ufundi lililopo chini ya Kocha Juma Mgunda ili kupata nafasi ya kucheza Jumapili.

Uongozi unahakikisha unalipa benchi la ufundi na wachezaji kila wanachohitaji ili kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo huo na kuwapa furaha Wanasimba.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER