Timu yaendelea kujifua Misri, Kagoma afunguka

Kikosi chetu kimeendelea na mazoezi leo kwa kufanya awamu moja tu ya jioni kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa mashindano hapa Ismalia Mısri.

Kesho kikosi chetu kinatarajia kucheza mchezo wa pili wa kirafiki saa 11:30 jioni dhidi ya El-Qanah utakaofanika Uwanja wa Old Suez Canal.

Baada ya mazoezi ya leo kiungo, Yusuph Kagoma amesema maandalizi yanayoendelea ni mazuri kwani wachezaji wanapata kila kitu wanachohitaji kwa wakati.

Kagoma amesema anawapongeza viongozi kwa kuchagua eneo sahihi na tulivyo kwa wachezaji kufanya maandalizi kwa ajili ya msimu ujao na anaamini kutokana na hilo tunakwenda kufanya vizuri.

Kagoma ameongeza kuwa kwenye kambi hii kuna viwanja vizuri, kuna gym bora, hali ya hewa nzuri, kuna bwawa zuri la kulitumia kwenye baadhi ya mazoezi ya kuweka miili sawa pamoja na vitu vyote sahihi vinavyohitajika kwa ajili maandalizi.

“Benchi letu lina makocha wazuri na ufundishaji wao mzuri. Wana mbinu nyingi wanazotupatia na hata mazoezi ya nguvu tunafanya mengi sahihi kwa ajili ya kuonyesha ushindani na viwango bora.”

“Kikubwa kazi na deni limebaki kwetu wachezaji kwenda kupambana kwenye kila mechi ili kupata ushindi kama malengo yetu yalivyo na kuwapa furaha mashabiki wetu,” amesema Kagoma.

 

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER