Kikosi chetu kimeondoka mchana kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kambi ya siku tatu kujiandaa na mechi zetu za Ligi Kuu ya NBC zilizosalia.
Tumeamua kuweka kambi Zanzibar kutokana na utulivu wake na tunaamini tutapata kile tulichokitarajia.
Tumesafiri na kikosi kizima cha wachezaji 28 kwa ajili ya kambi na lengo letu ni moja kuhakikisha tunafanya vizuri na kuibuka na alama zote tatu.
Tunafahamu itakuwa mechi ngumu na tunategemea kupata upinzani mkubwa lakini tunajiandaa kuwakabili.