Timu ya vijana yaendelea kufanya vizuri

Timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 imeibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa pili wa kundi A katika hatua ya nane bora.

Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu huku tukilisakama zaidi lango la Dodoma.

Dakika ya 18 nyota Luis Anthony alitupatia bao hilo pekee baada ya kupokea pasi kutoka kwa Isaya Ernest na kumtoka mlinzi na kumalizia mpira wavuni.

Huu ni mchezo wa pili wa timu ya vijana baada ya ule wa kwanza dhidi ya Ihefu tuliobuka na ushindi wa mabao 2-0 siku ya Jumatatu.

Matokeo haya yanatufanya kufuzu hatua ya nusu fainali huku tukiwa na mchezo mmoja mkononi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER