Timu kwenda Zanzibar kwa mwaliko maalumu

Kikosi chetu kitaondoka jijini Dar es Salaam kesho kutwa Ijumaa kuelekea Zanzibar kufuatia mwaliko tuliopewa na Shirikisho la Soka Visiwani humo (ZFF) ambapo tutacheza mechi mbili za kirafiki.

Mchezo wetu wa kwanza utakuwa Septemba 25 dhidi ya Kipanga FC utakaopigwa Uwanja Amani na mchezo wa pili utapigwa Septemba 27 katika Uwanja huo huo wa Amani ambapo mechi zote zitachezwa saa moja usiku.

Baada ya michezo hiyo miwili timu itarejea jijini Dar es Salaam Septemba 28.

Tayari kikosi kimeanza mazoezi leo kufuatia mapumziko ya siku mbili waliopewa wachezaji baada ya kumaliza mchezo wa hatua ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nyasa Big Bullets.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER